Wednesday, 26 September 2012

Mwanamke afugwa kwa miaka mitatu kwa uwizi wa mtoto

By Monica Okwany
Mwanamke mwenye umri wa  25 amepewa kifungo cha miaka mitatu baada ya kuiba mototo wa miaka miwili.
Irene Ayambuta alitekeleza wizi huo mnamo tarehe 18/9/2012 katika mtaa wa Oruba, kaunti ya Migori.
Bi Grace Wanyenyi Mutatiro alimwacha mwanawe Faith Wati akicheza na wenzake na kwenda sokoni kulangua parachichi na aliporudi alimkuta mtoto wake hayupo.
Aliambiwa na majirani kwamba mtoto wake alikuwa amechukuliwa na mwanamke ambaye hawakumtambua. Alimtafuta mtoto wake hadi nchi jirani ya Tanzania.
Alipata habari siku mbili baadaye kwamba mtoto wake alipatikana. Hapo ndipo wananchi walimvamia Bi Irene na kumpiga na kumjeruhi vibaya.
Aliokolewa na polisi ambao walimpeleka katika hospitali ya wilaya ya Migori kwa matibabu kabla ya kupelekwa korokoroni.
Alikubali mashtaka mbele ya hakimu mkaazi Bw. Edwin Nyaga ambaye alimpa kifungo cha miaka mitatu.
©KNA, Septemba 24, 2012

Mwanaume ashtakiwa kwa kosa la kuuza chang’aa

Na Monica Okwany

Mwanaume wa umri wa makamo alishtakiwa leo katika mahakama ya Migori kwa kosa la kuuza chang’aa kinyume cha sheria.

Roony Ochieng Alaka, alikamatwa mnamo tarehe 6/9/2012 akiendeleza biashara hiyo haramu katika kata ya Muhuru magharibi katika kaunti ya Migori.

Inadaiwa kuwa mshukiwa amekuwa akifanya biashara hiyo licha ya kuonywa na wanakijii ambao baadaye walimfahamisha naibu wa chifu wa eneo hilo bwana Julius Odhiambo.

Chifu huyo aliwaita maafisa wa polisi ambao walishirikiana na wanakijiji kufanya msako mkali na kupata lita 20 ya chang’aa iliyokuwa imehifadhiwa katika mifuko ya plastiki .

Kulingana na mkuu wa mashtaka Bi Dorcas Cherui, mshukiwa alikaidi sheria ya kujisajili kama muuzaji halali wa kinywaji hicho na kwamba hakuidhinishwa na tume ya kukadiria ubora wa bidhaa nchini,KEBS.

Aidha alipatikana na kosa la kuhifadhi kinywaji hicho kwenye kifaa cha plastiki ambacho kulingana na sheria hakijaidhinishwa na wizara ya afya na usafi.

Akielezea kisa hicho, bi cherui alionyenza pombe hiyo mbele ya mahakama kama.

Hata hivyo, mshukiwa alikubali makosa hayo na kuomba msamaha mbele ya hakimu mkuu Bw. David Kemei huku akijitetea kuwa alitekeleza biashara hiyo kujikimu kimaisha kwa kuwa hangeweza kufanya kazi nyingine ngumu kutokana na majeraha aliyopata kwenye ajali ya barabara.

Kesi hiyo itasikilizwa tarehe 12/9/2012.

Kwingineko Katika mahakama hiyo, Adericus Athiambo Oligi alishtakiwa kwa kosa la kupanda bangi katika kata ya Kadem Magharibi kinyume cha sheria.

Mshukiwa alipatikana akiwa amepanda mimea 25 ya bangi yenye thamani ya shilingi 2500 kwenye shamba lake.

Bwana Adericus alijitetea kwamba hakufahamu kuwa mimea hiyo ilikuwa ni bangi.

Kesi hiyo itasikizwa tarehe 18/9/2012.

©KNA, Migori Septemba 7, 2012