Friday, 15 February 2013

I AM FOR PEACE

Did I see people runnning?
were those men, women, and children?
can somebody explain to me the meaning of this confusion?
where did we go wrong... by casting a simple vote ?
 I am for peace.

today i stand for the many
who can not raise a word
because they think they are weak
and neglected
your rights make you strong
and have a place in our nation
I am for peace.

And was that your neighbor who stood up
against you?
did you not live in harmony at all times?
did you not graze together, eat and drink together?
is this some kind of a swine flu disease?
that makes people to stamble on children,
rape women and kill the old?
can somebody answer me?
I am for peace

now see where the bottle got broken,
the inciters, hate mongers and the
few who do not see the value of
maintaining peace.
this must stop
because we belong to one nation.
our nation Kenya

stand up for peace
in the 2013 elections
express your rights as kenyans
by casting your votes
...in peace

as for me , the future is bright
no more tears to shade
no more waillings
but a sign of rejoice and gladness
Wakenya tusimame imara na tuitetee amani ya nchi yetu
because I am for PEACE

Tuesday, 9 October 2012

Mazingira safi kupunguza magonjwa

Choo cha kuchimbwa kikitumiwa vizuri husaidia katika kupunguza ugonjwa wa kuhara pamoja na mkurupuko wa magonjwa mengine yanayotokana na uchafu wa mazingira.

Na Monica okwany

Swala la usafi ni sehemu muhimu katika maisha ya kila siku ya mwanadamu na inastahili kupewa kipaumbele ili kuepukana na magonjwa yanayozuka katika mazingira ya makazi ya binadamu. Hali hii ni kinyume katika wilaya ya Kuria Mashariki kwenye kaunti ya Migori ambapo usafi umepuuzwa kwa miaka mingi.

Asubuhi na mapema Bi Matilda Gati anaonekana akitoka katika nyumba yake ya vyumba viwili iliyoezekwa kwa nyasi akielekea kando na kuchutama kwenye kichaka yenye urefu wa mita kwenda haja ndogo .

Anatekeleza kitendo hicho akiwa na hofu ya kuonekana na mtu kwa sababu hana choo kilichochimbwa nyumbani mwake.

Wakati huo huo mita mia moja kutoka hapo, Bw. Peter Mosasi Mwita anadamka na kujitosa kwenye kichaka kilichoko nyuma ya nyumba yake na kuenda haja kubwa. Anachukua muda kujisafisha hali ambayo inachafua mazingira ya hewa safi kutokana na uchafu aliyouacha nyuma. Pia kwake kunakosekana choo cha nyumbani cha kuwezesha familia yake kujisaidia kwa njia ifaayo.

Mambo haya yanafanyika katika vitongoji vya eneo hilo na kuathiri mazingira yanayosababisha uchafuzi wa mito na makazi ya binadamu ambayo imesheheni uvundo unayotokana na kinyesi.

Uchafu unaotokana na mabaki ya vyakula na vinyesi imefanya wakaazi katika eneo hili kuhatarisha maisha ya wengi, kile kinachojulikana na wataalamu wa maswala ya afya kama ‘kusababisha vifo vya lazima kutokana na mkurupuko wa magonjwa yanayoweza kuzuilika.’

Wakaazi wa eneo hili wamekosa njia mwafaka ya kutupa taka kwa kisingizio cha kukosa vyoo vilivyochimbwa nyumbani.

Ni kwa sababu hii wizara ya afya ya umma na usafi ilijitolea kutoa mafunzo ya kipindi kifupi ili kuimarisha hali ya usafi katika vijiji kwa lengo la kupambana na udororaji wa usafi katika maeneo haya.

Hii kulingana na maafisa wa wizara hiyo itatekelezwa kwa ushirikiano na shirika lisilo la kiserikali la APHIA-PLUS mpanngo unaonuia kupata asilimia mia moja ya utumizi wa vyoo kwenye eneo hilo kufikia mwisho wa mwezi wa Agosti mwaka huu.
Afisa wa mradi huo Bw. James Otieno amesema kwamba uzinduzi wa mradi huo almaarufu kama “Community Led Total Sanitation (CLTS), itahakikisha kuwa kila nyumba katika eneo hilo inapata choo cha kutumia.

Kwa hivi sasa ukadiriaji wa vyoo katika wilaya hiyo ni asilimia 39.8 ambayo kulingana na wataalamu wa afya ni cha chini mno na kuweka wakaazi wa eneo hilo kwenye hatari ya kuambukizwa magonjwa ya kipindupindu na homa ya tumbo.

Bw Otieno katika mahojiano na KNA katika eneo hilo alisema utafiti uliofanyika hivi karibuni umeonyesha jinsi wakaazi wa eneo hilo walivyo kwenye hatari ya kuambukizwa magonjwa ya unywaji wa maji chafu inayotokana na uchafuzi wa hali ya juu ya mazingira kwa ujumla na vyanzo vya maji.

“Hali hii ndiyo imesababisha serikali kushirikiana na mashirika jirani kuhakikisha kwamba kila jamii imepata njia mwafaka ya kuhifadhi uchafu kwa kuwapa vifaa vifaavyo kwa matumizi hayo kwa sehemu zifaazo,” alidokeza haya wakati akizungumza na wanahabari katika afisi yake mjini Kegonga.
Afisa huyo alisema kwamba matumizi ya vyoo ni muhimu sana katika maisha ya wengi na mradi huo utaimarisha namna ya kuhifadhi uchafu unaotokana na shughuli za kibinadamu.
Mradi huo ambao kwa wakati huu umeanzishwa katika tarafa ya Kegonga umewapa zaidi ya nyumba 100 ambazo hazikuwa na vyoo vifaa muhimu katika miezi mitatu iliyopita.

“Tunanuia kufikia sehemu kama taarafa za Kwiho na Ntimaru kufikia mwanzo wa mwaka ujao,” Bw. Otieno amesema huku akitoa changamoto kwa wakaazi wa maeneo hayo kuwa na mazoea ya kutumia vyoo na kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa mazingira yao.

Japo mradi huo utakumbwa na changamoto ya kuwashawishi baadhi ya wakaazi wanaoshikilia dhana potovu kwamba kutumia vyoo husababisha vifo kama inavyoaminika na wengi.

Kwa wakaazi wengine kutumia choo kimoja katika familia moja ni kinyume na kaida za jamii na adhabu ya kwenda kinyume ni kifo.

“Maishani mwangu sijawahi kutumia choo kwa sababu ni hatia ambayo inaadhibiwa kwa kifo,” Bw Wantai Chacha alidai wakati akihojiwa.

“Unawezaje kutumia choo kimoja na watoto, wana na wakaza mwana wako na bado uwe na matumaini ya kuishi?” alishangaa Bw Chacha.
Kando na mila inayohusishwa na matumizi ya vyoo, kuna wale ambao wamekosa kuchimba vyoo majumbani mwao kutokana na hali ngumu ya kimaisha.

‘Ni ujinga kuharibu pesa katika kujenga choo wakati huna chumba cha kuishi,’ alisema Bw Gichoro katika mahojiano.

Baadhi ya wakaazi wa eneo hili ni wachochole kupindukia na wanaishi katika vyumba vikuu kuu vilivyoezekwa kwa nyasi na hivyo hawaoni haja ya kuwa na choo wakati kuna majani ambayo yamezingira majumba yao, alisema Bw Otieno.

“Lakini tumegundua kwamba wengi wa wakaazi wa eneo hilo ni wazembe na pia wamekosa kuhamasishwa kuhusiana na umuhimu wa kuwa na vyoo katika majumbani mwao,” aliongezea Bw Otieno.

Wednesday, 3 October 2012

Mwanamke afungwa miaka matatu kwa kumwiba mtoto wa miaka miwili

24 SEPTEMBA, 2012

NA MONICA OKWANY

Mwanamke mwenye umri wa makamo amepewa kifungo cha miaka mitatu baada ya kuiba mototo wa miaka miwili.

 Irene Ayambuta alitekeleza wizi huo mnamo tarehe 18/9/2012 katika mtaa wa Oruba, kaunti ya Migori.

 Bi Grace Wanyenyi Mutatiro alimwacha mwanawe Faith Wati akicheza na wenzake na kwenda sokoni kulangua parachichi na aliporudi alimkuta mtoto wake hayupo.

 Aliambiwa na majirani kwamba mtoto wake alikuwa amechukuliwa na mwanamke ambaye hawakumtambua. Alimtafuta mtoto wake hadi nchi jirani ya Tanzania.
 
Alipata habari siku mbili baadaye kwamba mtoto wake alipatikana. Hapo ndipo wananchi walimvamia Bi Irene na kumpiga na kumjeruhi vibaya.

Aliokolewa na polisi ambao walimpeleka katika hospitali ya wilaya ya Migori kwa matibabu kabla ya kupelekwa korokoroni.

Alikubali mashtaka mbele ya hakimu mkaazi Bw. Edwin Nyaga ambaye alimpa kifungo cha miaka mitatu.

Mvuvi afariki Migingo

Wavuvi katika kisiwa cha Migingo. Picha na Monica Okwany
TAREHE 21 SEPTEMBA

NA MONICA OKWANY.

Mwanamme mvuvi aliye na umri wa miaka 36 alizama katika kisiwa cha Migingo katika Ziwa Victoria kaunti ya Migori.

Mvuvi huyo anayetambulika kama Erick Ochieng Ouma alikumbana na kifo chake wakati akienda haja ndogo

Wenzake waliokuwa naye wamesema kwamba wakati marehemu alikuwa akienda haja ndogo, mawimbi makubwa yalizuka na kufanya mashua yao kutikisika hali iliyomfanya kuanguka majini.

Juhudi za kumsaka hazikufua dafu kwani mawimbi yalikuwa makali nayo giza nene ilikuwa imetanda.

Akithibitisha kisa hicho, mkuu wa polisi mjini Nyatike Bw Richard Bitonga alisema kwamba marehemu aliteleza kutoka kwa mashua waliokuwa wakitumia na wenzake watatu, na kuanguka ziwani.

Bw. Bitonga alitoa tahadhari kwa wavuvi katika eneo hilo kuwa makini katika shughuli zao na vilevile kuepuka matumizi ya madawa za kulevya wakati wakiwa baharini.

IEBC yazindua rasmi usajili wa wapiga kura kupitia njia ya kielektroniki

25septemba 2012
MONICA OKWANY

Tume huru ya uchaguzi na mipaka(IEBC) imeanza uhamasishaji wa umma kuhusiana na usajili wa wapiga kura kwa njia ya kielektroniki.

Afisa wa tume hiyo eneo bunge la Migori Bw. Mourice Raria, aliwasilisha ramani mpya ya maeneo ya kupiga kura.

Aliwataka wapiga kura kufahamu na kuelewa kodi zinazotumika kuwasilisha maeneo mapya na za awali ya kupiga kura katika kaunti ya Migori.

Alisema kwamba madhumuni ya mradi huo ni kuhakikisha kwamba ushirikiano katika usajili wa wapiga kura umeimarishwa.

Bw. Mourice aliongeza kuwa uwekezaji wa umeme utaimarishwa katika vituo vyote vya kupiga kura.

Akizungumza katika mkutano na wadau mjini Migori, Bw Mourice aliwahakikishia wapiga kura kuwa makarani wataelimishwa ipasavyo na kwa wakati huo huo hali ya usalama itaimarishwa katika vituo vyote vya upigaji kura kabla na baada ya kupiga kura.

Tume huru ya uchaguzi na mipaka inanuia kuwasajili wapiga kura 65000 katika maeneo bunge ya Suna Magharibi na Mashariki.

Baba aliyemnajisi bintiye wa miaka tisa atiwa kizuizini na polisi.

TAREHE 19 SEPTEMBA 2012

 NA MONICA OKWANY

Mwanamme wa umri wa makamo anazuiliwa katika kituo cha polisi huku uchunguzi ukiendelea kwa madai ya kumnajisi bintiye wa miaka tisa.

Bw Nicholas Abich alimnajisi bintiye mnamo tarehe 4/9/2012 wakati alikwenda kuchukua dawa aliyotumwa na mamake kutoka kwa nyumba.

Akithibitisha kisa hicho mkuu wa polisi mjini Migori Bw. Alfred Makoma alisema kwamba mwanaume huyo alimkamata bintiye na kumangusha kitandani mwao na kumfanyia kitendo hicho cha unyama.

“binti huyo alikimbia na kumweleza mamake ambaye alimjulisha chifu wa eneo la Rapon huko Awendo aliwaarifu polisi ambao walimtia mbaroni Nicholas” bw .Makoma alisema

Aidha bw. Makoma aliongeza kwamba visa kama hivi vimeongezeka sana katika maeneo ya migori akihoji kwamba uchunguzi unaendelea na iwapo mshukiwa atapatikana na hatia basi atachukuliwa hatua kali ya kisheria.

Wanafunzi wajeruhiwa baada ya ukuta wa shule kuporomoka

19/09/2012
NA MONICA OKWANY

Wanafunzi wanne wa shule ya msingi ya Pesoda wajeruhiwa baada ya ukuta unaozingira shule hiyo kuporomoka na kuwaangukia.

Akithibitisha kisa hicho mwalimu mkuu wa shule hiyo Bw Issac Maeri alisema kwamba ajali hiyo ilitokea mnamo saa 3.40 jioni wakati wanafunzi walikuwa michezoni.

Majeruhi walipelekwa katika hospitali jirani ya Oruba Nursing Home kwa huduma ya kwanza kabla ya kupelekwa katika hospitali ya misheni ya Ombo.

Kati ya wanafunzi walioumia ni wavulana wanne, watatu wakiwa katika darasa la tano na mmoja katika darasa la kwanza.

Wawili waliopata majeruhi madogo madogo walichukuliwa na wazazi wao na kupelekwa hospitalini kwa matibabu.

Mmoja alipata majeraha kichwani na mwingine mguuni .Wawili hao bado wako hospitalini lakini hali yao inaimarika .

Ajali hiyo ilisababishwa na shimo iliyokuwa ikichimbwa na hospitali ya ‘oruba nursing and maternty home’ kando ya ukuta wa shule hiyo.