Mwanaume wa umri wa makamo alishtakiwa leo katika mahakama ya Migori kwa
kosa la kuuza chang’aa kinyume cha sheria.
Roony Ochieng Alaka, alikamatwa mnamo tarehe 6/9/2012 akiendeleza biashara
hiyo haramu katika kata ya Muhuru magharibi katika kaunti ya Migori.
Inadaiwa kuwa mshukiwa amekuwa akifanya biashara hiyo licha ya kuonywa na
wanakijii ambao baadaye walimfahamisha naibu wa chifu wa eneo hilo bwana Julius
Odhiambo.
Chifu huyo aliwaita maafisa wa polisi ambao walishirikiana na wanakijiji
kufanya msako mkali na kupata lita 20 ya chang’aa iliyokuwa imehifadhiwa katika
mifuko ya plastiki .
Kulingana na mkuu wa mashtaka Bi Dorcas Cherui, mshukiwa alikaidi sheria
ya kujisajili kama muuzaji halali wa kinywaji hicho na kwamba hakuidhinishwa na
tume ya kukadiria ubora wa bidhaa nchini,KEBS.
Aidha alipatikana na kosa la kuhifadhi kinywaji hicho kwenye kifaa cha
plastiki ambacho kulingana na sheria hakijaidhinishwa na wizara ya afya na
usafi.
Akielezea kisa hicho, bi cherui alionyenza pombe hiyo mbele ya mahakama
kama.
Hata hivyo, mshukiwa alikubali makosa hayo na kuomba msamaha mbele ya
hakimu mkuu Bw. David Kemei huku akijitetea kuwa alitekeleza biashara hiyo
kujikimu kimaisha kwa kuwa hangeweza kufanya kazi nyingine ngumu kutokana na
majeraha aliyopata kwenye ajali ya barabara.
Kesi hiyo itasikilizwa tarehe 12/9/2012.
Kwingineko Katika mahakama hiyo, Adericus Athiambo Oligi alishtakiwa kwa
kosa la kupanda bangi katika kata ya Kadem Magharibi kinyume cha sheria.
Mshukiwa alipatikana akiwa amepanda mimea 25 ya bangi yenye thamani ya
shilingi 2500 kwenye shamba lake.
Bwana Adericus alijitetea kwamba hakufahamu kuwa mimea hiyo ilikuwa ni
bangi.
Kesi hiyo itasikizwa tarehe 18/9/2012.
©KNA, Migori Septemba 7, 2012
No comments:
Post a Comment