Wednesday, 3 October 2012

IEBC yazindua rasmi usajili wa wapiga kura kupitia njia ya kielektroniki

25septemba 2012
MONICA OKWANY

Tume huru ya uchaguzi na mipaka(IEBC) imeanza uhamasishaji wa umma kuhusiana na usajili wa wapiga kura kwa njia ya kielektroniki.

Afisa wa tume hiyo eneo bunge la Migori Bw. Mourice Raria, aliwasilisha ramani mpya ya maeneo ya kupiga kura.

Aliwataka wapiga kura kufahamu na kuelewa kodi zinazotumika kuwasilisha maeneo mapya na za awali ya kupiga kura katika kaunti ya Migori.

Alisema kwamba madhumuni ya mradi huo ni kuhakikisha kwamba ushirikiano katika usajili wa wapiga kura umeimarishwa.

Bw. Mourice aliongeza kuwa uwekezaji wa umeme utaimarishwa katika vituo vyote vya kupiga kura.

Akizungumza katika mkutano na wadau mjini Migori, Bw Mourice aliwahakikishia wapiga kura kuwa makarani wataelimishwa ipasavyo na kwa wakati huo huo hali ya usalama itaimarishwa katika vituo vyote vya upigaji kura kabla na baada ya kupiga kura.

Tume huru ya uchaguzi na mipaka inanuia kuwasajili wapiga kura 65000 katika maeneo bunge ya Suna Magharibi na Mashariki.

No comments:

Post a Comment