| Wavuvi katika kisiwa cha Migingo. Picha na Monica Okwany |
NA MONICA OKWANY.
Mwanamme mvuvi aliye na umri wa miaka 36 alizama katika
kisiwa cha Migingo katika Ziwa Victoria kaunti ya Migori.
Mvuvi huyo anayetambulika kama Erick Ochieng Ouma alikumbana
na kifo chake wakati akienda haja ndogo
Wenzake waliokuwa naye wamesema kwamba wakati marehemu
alikuwa akienda haja ndogo, mawimbi makubwa yalizuka na kufanya mashua yao
kutikisika hali iliyomfanya kuanguka majini.
Juhudi za kumsaka hazikufua dafu kwani mawimbi yalikuwa
makali nayo giza nene ilikuwa imetanda.
Akithibitisha kisa hicho, mkuu wa polisi mjini Nyatike Bw
Richard Bitonga alisema kwamba marehemu aliteleza kutoka kwa mashua waliokuwa wakitumia
na wenzake watatu, na kuanguka ziwani.
Bw. Bitonga alitoa tahadhari kwa wavuvi katika eneo hilo
kuwa makini katika shughuli zao na vilevile kuepuka matumizi ya madawa za
kulevya wakati wakiwa baharini.
No comments:
Post a Comment