NA MONICA OKWANY
Mwanamme wa umri wa makamo
anazuiliwa katika kituo cha polisi huku uchunguzi ukiendelea kwa madai ya
kumnajisi bintiye wa miaka tisa.
Bw Nicholas Abich alimnajisi
bintiye mnamo tarehe 4/9/2012 wakati alikwenda kuchukua dawa aliyotumwa na
mamake kutoka kwa nyumba.
Akithibitisha kisa hicho mkuu
wa polisi mjini Migori Bw. Alfred Makoma alisema kwamba mwanaume huyo
alimkamata bintiye na kumangusha kitandani mwao na kumfanyia kitendo hicho cha
unyama.
“binti huyo alikimbia na
kumweleza mamake ambaye alimjulisha chifu wa eneo la Rapon huko Awendo
aliwaarifu polisi ambao walimtia mbaroni Nicholas” bw .Makoma alisema
Aidha bw. Makoma aliongeza
kwamba visa kama hivi vimeongezeka sana katika maeneo ya migori akihoji kwamba
uchunguzi unaendelea na iwapo mshukiwa atapatikana na hatia basi atachukuliwa
hatua kali ya kisheria.
No comments:
Post a Comment