NA MONICA OKWANY
Wanafunzi
wanne wa shule ya msingi ya Pesoda wajeruhiwa baada ya ukuta unaozingira shule
hiyo kuporomoka na kuwaangukia.
Akithibitisha
kisa hicho mwalimu mkuu wa shule hiyo Bw Issac Maeri alisema kwamba ajali hiyo
ilitokea mnamo saa 3.40 jioni wakati wanafunzi walikuwa michezoni.
Majeruhi
walipelekwa katika hospitali jirani ya Oruba Nursing Home kwa huduma ya kwanza
kabla ya kupelekwa katika hospitali ya misheni ya Ombo.
Kati
ya wanafunzi walioumia ni wavulana wanne, watatu wakiwa katika darasa la tano
na mmoja katika darasa la kwanza.
Wawili
waliopata majeruhi madogo madogo walichukuliwa na wazazi wao na kupelekwa
hospitalini kwa matibabu.
Mmoja
alipata majeraha kichwani na mwingine mguuni .Wawili hao bado wako hospitalini
lakini hali yao inaimarika .
Ajali
hiyo ilisababishwa na shimo iliyokuwa ikichimbwa na hospitali ya ‘oruba nursing
and maternty home’ kando ya ukuta wa shule hiyo.
No comments:
Post a Comment