Mwanamme wa umri wa miaka 63
hivi leo amefikishwa mbele ya mahakama ya Migori akikabiliwa na kosa la wizi wa
kimabavu.
James Leparan Naiyioma
anadaiwa kuwa mnamo tarehe 16/1/2011 katika mtaa wa Ranen wilayani Migori,
akishirikiana na wengine ambao hawakuwa mahakamani walikuwa wamejihami kwa
silaha hatari zikiwemo bunduki, panga na rungu walimvamia Bw. Richard Kones
Oyer na kumwibia mali yake ikiwemo nguo, redio aina ya sony, busta ya runinga,
simu za rununu 12, ‘ airtime voucher’ yenye thamani ya shilingi 60 000 na pesa
taslimu shilingi 227 000.
Hata hivyo Bw. Leparan
alikanusha mashtaka hayo mbele ya hakimu mkaazi Bw Edwin. M. Nyaga.
Aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi
100 000 na udhamini wa kiasi hicho.
Kesi hiyo itasikizwa tarehe
29/10/2012.
No comments:
Post a Comment