Na Monica Okwany
Mwanamme aliye na umri wa
miaka 21 amefungwa kwa kosa la kumiliki misokoto mitano ya bangi huku mwingine
ashtakiwa kwa kulaghai mwenzake shilling 249,000.
Duncan Onyango Ochieng alifikishwa
mbele ya hakimu mkaazi Bi Grace Kiruguma mnamo tarehe 10/09/2012 na kushtakiwa
kwa kosa la kuhifadhi bangi yenye gramu 50 iliyo na thamani ya shilingi 50.
kinyume cha sheria nambari 4 sehemu ya 3 ya mwaka wa1994 .
Akielezea mahakama, mkuu wa
mashtaka Bw.G Kimani alisema kwamba mshukiwa alitiwa mbaroni na babake mzazi
Bw. Ochieng Ouya aliyesaidiwa na wanakijiji baada ya kuteketeza nyumba yao
katika kata ya Mapera kaunti ya Migori.
Mshukiwa ambaye ni mkulima
katika kata ndogo ya Got Jope Abila, alishikwa na kufanyiwa msako na wanakijiji
ambapo misokoto mitano ya bangi ilipatikana ndani ya mfuko wake wa suruali
ndefu.
Mahakama ilimpata na hatia na
kumpa kifungo cha mwaka mmoja.
Kwingineko katika mahakama
hiyo mwanamme aliye na umri wa miaka 41 alifikishwa mbele ya hakimu mkaazi Bi
Grace Kirugumi mnamo tarehe 10/09/2012 kwa kosa la kumlaghai Bw Rodgers Abisai
shilingi 249 000 tarehe 2/06/2011 kwa madai ya kuteuliwa na kupewa mamalaka ya
kuchunguza na kumiliki mali ya marehemu Bw. George Riogi Motende.
Mshukiwa ambaye alitambuliwa
kama Bw. Robert Gideon Onderi alipatikana na hatia ya kuchukua pesa kwa njia ya
ulaghai kinyume cha sheria.
Pia, alipatikana na hatia ya
kutoa ushahidi wa uongo tarehe 2/7/2009 mbele ya hakimu Bw. Kibet Samba kwa
kuapa kuwa alikuwa nduguye marehemu Bw.George Rioyi Molende ili kupata barua ya
urithi wa mali ya marehemu.
Mshukiwa ambaye ni mkaazi wa
mtaa wa Nyamesango wilaya ya Gucha mjini Kisii bado anazuiliwa huku uchunguzi
ukiendelea.
No comments:
Post a Comment