Na Monica Okwany
Mwanamke wa umri wa miaka 36
anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Awendo kwa kosa la kumdhulumu kimapenzi
mvululana wa miaka 17.
Carolyn Atieno alikamatwa
mnamo tarehe nne mwezi wa tisa mwaka huu katika kijiji cha ominde akimdhulumu
George oliech , mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi ya Awendo.
Akithibitisha kisa hicho,
mkuu wa polisi mjini Migori bw. Alfred Makoma alisema kwamba mshukiwa alifumaniwa
akitekeleza kitendo hicho chumbani mwake.
Bw .makoma alisema mwanamke
huyu alimwalika kijana huyu chumbani kwake kwa madai ya kumpa kikombe cha chai
na hapo ndipo mshukiwa alimshawishi kijana huyo na kumvua nguo huku akimshika
bila ruhusa yake na kumlazimisha kufanya mapenzi naye.
Kijana huyu aliokolewa na
majirani ambao walipiga kamsa na kuwaita watu ambao walikusanyika na kumfumania
peupe akila uroda na kijana huyo kinyume na sheria.
Akizungumza na wanahabari,
bw. Makoma alisema kuwa vitendo kama hivi vimeongezeka katika maeneo ya Migori
na Awendo.
Alitoa onyo kwa wakaazi wa
eneo hilo kuwa makini na kupiga ripoti kwa polisi ama idara husika ili hatua za
kisheria zichukuliwe kwa watu kama hao.
Aidha bw. makoma alitoa mwito
kwa wakaazi wa eneo hilo kuheshimu maslahi ya vijana na watoto hasa wa shule
ili kujenga maisha yao ya siku za usoni.
No comments:
Post a Comment